CHUNYA TOBACCO GROWERS COOPERATIVE UNION

( CHUTCU )

Historia na Uhai Wa Chama

Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku Chunya (CHUTCU LTD) ni muungano wa Vyama vya Ushirika vya Msingi vinavyolima zao la biashara la Tumbaku Chunya na Songwe pamoja na mazao ya chakula. Chama hiki kiliandikishwa katika Daftari la Serikali tarehe 20/09/2000 kwa matazamio na hatimaye kupata usajili wa kudumu tarehe 30/01/2003. Chama Kikuu mpaka sasa kina jumla ya Vyama wanachama hai 30 kutoka wilaya za Chunya na Songwe na Ofisi za Chama Kikuu zipo Chunya Mjini, Mkoa wa Mbeya.

Dira yetu

Dira ya CHUTCU Ltd ni kutoa huduma bora kwa vyama vya ushirika wanachama kwa kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa na vyama hivyo na kuhakikisha uboreshaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya wanachama wao

Dhamira

Dhamira ya CHUTCU Ltd ni kuboresha huduma kwa vyama wanachama na kuhakikisha kuwa wanazalisha tumbaku yenye ubora wa juu ili kupata bei nzuri ya kuvutia kwa ajili ya maendeleo yao ya kiuchumi

Shughuli za Chama Kikuu

Shughuli za Chama Kikuu ni kustawisha hali ya wanachama wake kwa kufanya mipango ya kuendeleza shughuli za kilimo zinazoendeshwa na vyama vilivyojiunga pamoja na wanachama wake kwa kufuata misingi na taratibu za vyama vya Ushirika na sheria ya ushirika Na. 6 ya mwaka 2013, hasa kwa kufanya mambo yafuatayo:-

  1. Kuwa wakala wa kukusanya, kuhifadhi, pamoja na kutafuta soko la mazao ya tumbaku, alizeti, mahindi, korosho na mazao mengine kwa lengo la kuyauza kwa bei nzuri kwa faida ya wanachama wake.
  2. Kununua, kuuza na kusambaza pembejeo za kilimo kwa wanachama wake kwa bei nafuu ili kuboresha mazao ya biashara na chakula.
  3. Kutoa Elimu ya Ushirika kwa wanachama wake na kuwaendeleza kielimu watendaji wa chama kikuu.
  4. Kuanzisha na kuendeleza mitandao mizuri na imara ya kilimo bora cha tumbaku na mazao mengine,
  5. Pia, kufanya shughuli nyingine zilizohalali na ambazo hazivunji sheria za nchi kama ni vile kuanzisha viwanda vidogo vidogo na vikubwa katika kuendeleza kazi zilizotajwa hapo juu kwa kufuata kanuni, masharti ya chama na sheria ya vyama vya ushirika Na.6 ya mwaka 2013 inavyoelekeza sambamba na Kanuni zake za mwaka 2015.

Jiandikishe kwa Barua pepe zetu

Habari Mpya

Vifaa Tiba

Ugeni wa Mkuu wa Wilaya

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mayeka S. Mayeka amepokea vitanda vitatu kwa ajili ya kujifungulia akina Mama, kufanyia upasuaji na kulazia wagonjwa pamoja na

Read More »
Vifaa Tiba

Ugeni wa Mkuu wa Wilaya

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mayeka S. Mayeka amepokea vitanda vitatu kwa ajili ya kujifungulia akina Mama, kufanyia upasuaji na kulazia wagonjwa pamoja na

Read More »
Vifaa Tiba

Ugeni wa Mkuu wa Wilaya

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mayeka S. Mayeka amepokea vitanda vitatu kwa ajili ya kujifungulia akina Mama, kufanyia upasuaji na kulazia wagonjwa pamoja na

Read More »
Uzalishaji

Taarifa

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua. Ut enim ad minim veniam, quis

Read More »