Kuhusu CHUTCU
Historia na Uhai Wa Chama
Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku Chunya (CHUTCU LTD) ni muungano wa Vyama vya Ushirika vya Msingi vinavyolima zao la biashara la Tumbaku Chunya na Songwe pamoja na mazao ya chakula. Chama hiki kiliandikishwa katika Daftari la Serikali tarehe 20/09/2000 kwa matazamio na hatimaye kupata usajili wa kudumu tarehe 30/01/2003. Chama Kikuu mpaka sasa kina jumla ya Vyama wanachama hai 30 kutoka wilaya za Chunya na Songwe na Ofisi za Chama Kikuu zipo Chunya Mjini, Mkoa wa Mbeya.
Dira yetu
Dira ya CHUTCU Ltd ni kutoa huduma bora kwa vyama vya ushirika wanachama kwa kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa na vyama hivyo na kuhakikisha uboreshaji wa maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya wanachama wao
Dhamira
Dhamira ya CHUTCU Ltd ni kuboresha huduma kwa vyama wanachama na kuhakikisha kuwa wanazalisha tumbaku yenye ubora wa juu ili kupata bei nzuri ya kuvutia kwa ajili ya maendeleo yao ya kiuchumi
Benki zetu
CHUTCU LTD mpaka sasa inafanya biashara ya taasisi za kifedha/benki nne (4) ambazo zinatoa mikopo kwa wakulima wa tumbaku waliopo katika Vyama vya Msingi (AMCOS) 30 katika Mkoa wa kitumbaku Chunya. Benki hizo ni;
- CRDB PLC
- AZANIA BANK
- NBC LIMITED
- NMB PLC
Ujenzi wa Kiwanda
CHUTCU Ltd katika kuunga mkono jitahada za serikali imejenga kiwanda chenye mitambo ya kusaga unga wa nafaka inayotokana na mahindi pamoja na kufunga mtambo wa kukamua mafuta ya alizeti ili kuongeza thamani ya mazao yanayolimwa na wakulima wilayani Chunya. Mradi huu mpaka kukamilika unatarajia kutumia kiasi cha shilingi 367,657,726.63 ambapo kiasi hiki kitahusisha Shilingi 74,000,000 ununuzi wa mtambo wa kusaga unga, na kiasi cha shilingi 29,960,000 ikiwa ni ununuzi wa mtambo wa kukamua mafuta ya alizeti. Mitambo yote hii miwili imenunuliwa SIDO (Shirika la Maendeleo ya Viwanda Vidogo) na gharama za ujenzi wa jengo ni shilingi 262,697,726.63.
Uongozi
Bodi ya CHUTCU LTD
S/N | JINA | WADHIFA |
1 | Sebastian Masika | Mwenyekiti |
2 | Elieza Fijaboh | Makamu |
3 | Alberto Kacheza | Mjumbe |
4 | Violet Kawemba | Mjumbe |
5 | Yona Chawene | Mjumbe |
6 | Isaya Daniel | Mjumbe |
7 | Epimarcus Sikumoja | Mjumbe |
8 | Thomas Mgalula | Mjumbe |
MENEJIMENTI
S/N | JINA | WADHIFA |
1 | Christian Msigwa | Meneja Mkuu |
2 | Juma Nshinshi | Meneja Shughuli |
3 | Daniel Mpigasupi | Mkaguzi wa Ndani |
4 | Francisco Chidege | Mhasibu |
IDARA ZA MENEJIMENTI
- Idara ya Utawala
- Idara ya Uzalishaji na Masoko
- Idara ya Ukaguzi wa Ndani
- Idara ya Uhasibu