You are currently viewing Ugeni wa Mkuu wa Wilaya

Ugeni wa Mkuu wa Wilaya

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mayeka S. Mayeka amepokea vitanda vitatu kwa ajili ya kujifungulia akina Mama, kufanyia upasuaji na kulazia wagonjwa pamoja na mashuka 20 vyenye thamani ya Shilingi Milioni Nne kutoka Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku Chunya (CHUTCU Ltd) katika Kituo cha Afya Lupa kilichopo wilayani Chunya Mkoa wa Mbeya

Mwenyekiti wa Bodi ya CHUTCU LTD Bw. Sebastian Masika akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Bodi kwa Mkuu wa Wilaya amesema kuwa wameanza kutekeleza matakwa ya Misingi ya Ushirika ya kujali jamii na kurudisha fadhila kwa kuchangia shughuli za kijamii hasa katika suala la afya kwa sababu kilimo hakiwezi kufanyika kama afya ya wakulima na wananchi ikiwa dhohofu

Aidha Meneja Mkuu wa CHUTCU LTD Bw. Christian Msigwa alisema kuwa wameanza kufanya jambo hili la kujali jamii katika Kituo cha Afya Lupa ikiwa eneo muhimu na kitovu cha Vyama vya Msingi (AMCOS) vingi wilayani Chunya lakini zoezi hili litakuwa endelevu kila mwaka na pale itakapohitajika kuchangia watakuwa wakifanya hivyo ili kuhakikisha wakulima wa tumbaku wanajivua uwepo wa CHUTCU Ltd

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Lupa Bw. Obeid Prosper ametoa kubwa sana kwa CHUTCU LTD kwa kuwaletea msaada wa vifaa hivyo kwani walikuwa na upungufu wa vitanda kituoni hapo ambapo vitasaidia sana kupinguza changamoto hiyo. Aidha, amewaomba kuendelea na moyo huo wa kugusa afya za wananchi ambao ndiyo wakulima wao wa tumbaku Chunya.

Wakati huo huo DC Mayeka amewapongeza CHUTCU Ltd kwa kujenga kiwanda cha kusaga unga wa mahindi na kukamua mafuta ya alizeti na kuwahakikishia kuwa serikali itakuwa inawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao kwani kwa mwaka wa fedha huu Halmashauri ya wilaya ya Chunya imepata mapato ya zaidi ya Bilioni 2.8 kutokana na ushuru wa tumbaku, hivyo lazima watambue mchango wa watu wanaosimamia zao hilo la tumbaku

Leave a Reply